Home » Video » Dkt. Hamisi Kigwangalla ametoa siku tatu kwa uongozi wa Hospitali yaTumbi

Dkt. Hamisi Kigwangalla ametoa siku tatu kwa uongozi wa Hospitali yaTumbi

News Category: 
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla ametoa siku tatu kwa uongozi wa Hospitali ya teule ya rufaa ya Mkoa wa Pwani-Tumbi kufunga chumba cha kuhifadhi maiti (Mochwari) baada ya kubaini matatizo mbalimbali baada ya kufanya ziara katika hospitali hiyo.
 
Katika ziara hiyo, Dk. Kigwangalla alibaini mambo mbalimbali kutoenda sawa ikiwemo suala la utendaji mbovu ambapo alitoa agizo la kumtaka Mkurugenzi wa Shirika la Elimu Kibaha wanaosimamia Hospitali hiyo kutoa maelezo ndani ya masaa 24 kama anafaa kubaki ama la!.
 
Aidha, Dk. Kigwangalla amebainisha kuwa, hali aliyoikuta katika chumba cha kuhifadhia maiti ni mbaya hivyo ilikuondoa matatizo amelazimika kuifunga kwa muda huo wa siku tatu ilikufanyia marekebisho kwa baadhi ya mambo ndani ya chumba hicho cha mochwari hospitalini hapo.
 
Awali vyombo vya habari vilitoa hiyo ikiwemo badhi ya maiti kuhifadhiwa nje na kuatarisha afya za wananchi.
 
Ad