Home » Tanzania » Majokofu chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya rufaa ya Tumbi, hayafanyi kazi

Majokofu chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya rufaa ya Tumbi, hayafanyi kazi

04 March 2016 | Tanzania

Majokofu Maalumu ya chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya rufaa ya Tumbi, hayafanyi kazi kwa muda wa siku nne sasa, hali ambayo imesababisha usumbufu mkubwa kwa wafiwa wanaopeleka maiti zao katika hospitali hiyo.

Bi Eda Lemba Muhama ni Mmoja ya ndugu ambaye alifika kwenye hospitali hiyo kwa ajili ya kuuchukua mwili wa ndugu yake aliyefariki hivi karibuni. Anasikitishwa na hali aliyoikuta huku mwili wa ,pemdwa wake ukiwa umelazwa katika sakafu iliyotapakaa funza wanaotoka kwenye miili iliyoharibika.

Kwa upande wake Mtumwa Eid ni mmoja kati ya wahudumu wa kitengo cha kuhifadhia maiti katika hospitalini hiyo kwa miaka 20, amesema kutokana na udogo wa chumba hicho kunawalazimu kuweka miiili miwili katika kasha moja, jambo ambalo kinyume na utaratibu, lakini pia mazingira duni ya chumba hicho ambayo kumetajwa kuhatarisha hali ya afya wahudumu hao

Ad