Home » Tanzania » Watumishi hewa 2,702; nchi nzima

Watumishi hewa 2,702; nchi nzima

31 March 2016 | Tanzania
MKOA Mwanza waongoza kuwa na watumishi  hewa 334  ukifuatiwa na Mkoa wa Arusha kwa kuwa na watumishi hewa 270 ikiwa nchi nzima na watumishi  hewa 2,702.

Hata hivyo Shinyanga na Songwe ni mikoa isiyo  na watumishi hewa kutokana na mikakati ya mikoa hiyo kila idara kupeleka majina ya watu wanaostahili kulipwa mishahara kila mwezi.

 
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Anne Killango amesema kuwa viongozi walioanza katika mikoa huo walijipanga katika kuondokana na watumishi hewa.
 
kukosekana kwa watumishi hewa katika Mkoa wa Songwe   kunatokana na upya wake na mkuu wake mkoa ameapishwa hivi karibuni.
 
Akizungumza na Wakuu wa Mikoa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, George Simbachawene aliwataka wakuu wa mikoa wafanye kazi ikiwemo ubunifu wa miradi ya kuongeza mapato.
 
Simbachawene amewataka wakuu wa mikoa kuondokana na matumizi yasio na lazima ili fedha hizo zitumike katika matumizi ya msingi.
 
Amesema kuwa zoezi hilo liweze kuwa endelevu ikiwa ni pamoja na kushughulika na watoro ambao wanalipwa fedha wakati hawafanyi kazi,
Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri amesema wote ambao wamehusika na hujuma za mishahara wafikishwe katika vyombo vya dola na mkoa wake umeanza kutekeleza.
Mkuu wa Mkoa wa Lindi ,Godfrey Zambi akikabidhi majina ya watumishi hewa kwa Waziri wa nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, George Simbachawene
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam  akizungumza Waziri wanchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, George Simbachawene  baada ya kumkabidhi majina watumishi hewa 
 
 
Ad