Home » Tanzania » Wakuu wa mikoa na wilaya watakiwa kutoa taarifa ya upungufu wa vitanda hospitalini

Wakuu wa mikoa na wilaya watakiwa kutoa taarifa ya upungufu wa vitanda hospitalini

15 February 2016 | Tanzania

Waziri wa maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto UMMY MWALIMU, amewaagiza wakuu wa mikoa na wilaya kote nchini kutoa taarifa ya upungufu wa vitanda katika hospitali za serikali zilizopo katika maeneo yao ili serikali iendelee kuboresha huduma za afya

Waziri MWALIMU ametoa aagizo hilo katika hospitali ya Taifa Muhimbili jijini DSM, wakati kipokea vitanda na magodoro vyenye thamani ya Shilingi Milioni 88.7 kwa ajili ya wodi mpya ya wazazi kufuatia agizo la Rais Dkt. JOHN MAGUFULI.

Katika hatua nyingine Waziri MWALIMU ametoa agizo la kusimamishwa kazi kwa baadhi ya watendaji wa MSD kutokana na ubadhilifu wa fedha. 

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa MSD, LAUREN BWANAKUNU amesema MSD, imetoa vitanda 120, magodoro 120, vitanda maalum kwa watoto wadogo KUMI, vitanda vya kujifungulia KUMI na mashuka 480 vyote vikiwa na thamani ya Shilingi Milioni 88.7.

Ad