Home » Tanzania » Uteuzi wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu NSSF Dkt. Carina Wangwe watenguliwa

Uteuzi wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu NSSF Dkt. Carina Wangwe watenguliwa

03 March 2016 | Tanzania

Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mheshimiwa Jenister Joakim Mhagama ametengua uteuzi wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Dkt. Carina Wangwe uliotangazwa leo Jijini Dar es salaam.

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa usiku huu, imeeleza kuwa uteuzi huo umetenguliwa kutokana na kutokamilika kwa baadhi ya taratibu.

Kulingana na Taarifa hiyo, uteuzi mpya kwa mujibu wa mamlaka na sheria utakapofanyika taarifa zitatolewa kwa wananchi

Ad