Home » Tanzania » TANZANIA NA KUWAIT ZAJADILI UDHIBITI WA MIPAKA

TANZANIA NA KUWAIT ZAJADILI UDHIBITI WA MIPAKA

12 February 2019 | Tanzania

 

PIX 1
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza
 na  Balozi  wa  Kuwait nchini, Mubarak Mohamed Alsehaijan (kulia),  juu  ya  
kubadilishana  uzoefu katika Udhibiti  wa  Mipaka. Mazungumzo hayo yamefanyika leo,
Ofisi Ndogo ya wizara, jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
PIX 2
Balozi wa Kuwait nchini, Mubarak Mohamed Alsehaijan, akizungumza na
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni   juu ya
kubadilishana  uzoefu  katika  Udhibiti wa Mipaka.Mazungumzo hayo yamefanyika leo,
Ofisi  Ndogo  ya  wizara, jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
PIX 3
Balozi wa Kuwait Nchini, Mubarak Mohamed Alsehaijan  akisaini Kitabu cha
Wageni baada ya kuwasili Ofisi Ndogo ya Wizara ya Mambo ya ndani ya Nchi,
jijini Dar es Salaam. Kushoto ni  Naibu Waziri wa wizara hiyo, Mhandisi Hamad
Masauni.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
PIX 4
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,  Mhandisi  Hamad  Masauni, akiagana
na Balozi wa Kuwait nchini, Mubarak Mohamed Alsehaijan (kulia), baada ya
kumaliza mazungumzo yaliyohusu kubadilishana uzoefu katika Udhibiti wa Mipaka.
Mazungumzo  hayo  yamefanyika leo, Ofisi  Ndogo ya wizara, jijini Dar es Salaam.
Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 

 

Serikali ya Tanzania na Nchi ya Kuwait ziko katika mpango maalumu wa kubadilishana uzoefu juu ya udhibiti wa mipaka ikiwa ni juhudi za Tanzania kuimarisha ulinzi katika mikoa yote nchini iliyopo mipakani
 
Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni wakati wa mazungumzo na Balozi wa Kuwait Nchini, Mubarak Mohamed Alsehaijan ikiwa ni mpango wa nchi hizo kubadilishana uzoefu katika kudhibiti uhalifu katika mikoa ya mipakani
“Kama Serikali tuna vipaumbele katika kudhibiti  mipaka yetu kutokana na uhalifu unaotokea ikiwemo wahamiaji haramu,usafirishaji wa binadamu, uingiaji wa silaha,utoroshwaji wa madini na biashara yamagendo, ndio maana tumekutana leo kujadili ushirikiano wa nchi hizi mbili katika kudhibiti uhalifu huo”alisema Masauni
 
Akizungumza katika kikao hicho Balozi wa Kuwait Nchini, Mubarak Mohamed Alsehaijan alisema Tanzania ni nchi salama na wameamua kubadilishana uzoefu katika usimamiaji na udhibiti  wa mipaka.
“Tuna uhusiano mzuri baina ya Kuwait na Tanzania,tumekubaliana kubadilisha uzoefu ili kuweza kuimarisha sekta ya ulinzi kwa kutumia teknolojia itakayorahisisha udhibiti wa mipaka hapa nchini Tanzania” alisema Balozi Mubarak
 
Katika mazungumzo hayo pia walijadili juu ya teknolojia ya udhibiti wa majanga ikiwemo moto na ajali ambapo pia ni eneo ambalo nchi hizo mbili zilishaanza kushirikiana katika shughuli za uokozi.
Ad