Home » Tanzania » Rais wa Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein amemuapisha Balozi Seif Ali Iddi kuwa Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar

Rais wa Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein amemuapisha Balozi Seif Ali Iddi kuwa Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar

31 March 2016 | Tanzania

Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi(kushoto) akiwa na Viongozi waliohudhuria kuapishwa kwake ,(wa pili kushoto) Katibu Mkuu Kiongozi Dkt.Abdulhamid Yahya Mzee,Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi na Naibu Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Mahmoud Mussa Wadi.

Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe,Zubeir Ali Maulid akiwa na Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe,Omar Othman Makungu (kushoto) wakati wa kuapishwa Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kushika nafasi hiyo  Ikulu Mjini Zanzibar.

Mwanasheria Mkuu wa zanzibar Mhe,Said Hassan Said (kushoto) Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe,Omar Othman Makungu (katikati) na Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe,Zubeir Ali Maulid wakiwa katika hafla ya kuapishwa Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kushika nafasi hiyo  Ikulu Mjini Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na Mama Asha Suleiman Iddi baada ya kumuapisha Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar  katika hafla iliyofanyika leo Ikulu Mjini Zanzibar,(Picha na Ikulu.]

 

Ad