Home » Tanzania » Rais wa Jamhuri ya Chad Mhe. Idriss Deby Itno amewasili hapa nchini kwa ziara kikazi ya siku 2

Rais wa Jamhuri ya Chad Mhe. Idriss Deby Itno amewasili hapa nchini kwa ziara kikazi ya siku 2

27 November 2016 | Tanzania

Rais wa Jamhuri ya Chad Mhe. Idriss Deby Itno leo tarehe 27 Novemba, 2016 majira ya alasiri amewasili hapa nchini kwa ziara kikazi ya siku 2.

Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam Rais Idriss Deby Itno akiwa na Mkewe Mama Hinda Deby amepokelewa na mwenyeji wake Rais Magufuli na kisha kulakiwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa na wananchi.

Rais Magufuli amefanya mazungumzo na Rais Idriss Deby Itno Ikulu Jijini Dar es Salaam.

 

 

Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Dar es Salaam

27 Novemba, 2016

Ad