Home » Tanzania » RAIS MAGUFULI kuanza ziara yake ya kwanza mkoani DODOMA

RAIS MAGUFULI kuanza ziara yake ya kwanza mkoani DODOMA

16 November 2015 | Tanzania

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta JOHN MAGUFULI anatarajiwa kwa mara ya kwanza kuwasili Makao Makuu ya nchi Mjini DODOMA kwa ziara rasmi ya kikazi.

Katika ziara hiyo Rais MAGUFULI pamoja na mambo mengine anatarajiwa kuzindua Bunge la Kumi na Moja na kupendekeza jina la Waziri Mkuu wake.

Pia kikao hicho cha kwanza cha Bunge la Kumi na Moja kitapata nafasi ya kumchagua Spika wake mpya atakayesimamia shughuli za bunge kwa Miaka MITANO ijayo

Ad