Home » Tanzania » Rais Magufuli awathibitisha watendaji wakuu wa taasisi mbili za Serikali

Rais Magufuli awathibitisha watendaji wakuu wa taasisi mbili za Serikali

13 March 2016 | Tanzania

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewathibitisha watendaji wakuu wa taasisi mbili za serikali.

Waliothibitishwa ni Bw. Alphayo Kidata, aliyekuwa Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), ambaye anakuwa Kamishna Mkuu wa TRA, na

Bw. Valentino Mlowola aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), ambaye anakuwa Mkurugenzi Mkuu wa (TAKUKURU).

Watendaji hawa wamethibitishwa kuanzia leo tarehe 13 Machi, 2016

 

Gerson Msigwa

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mawasiliano, IKULU.

Dar es salaam

13 Machi, 2016

Ad