Home » Tanzania » Rais Magufuli amteua Waziri Mkuu Mstaafu Pinda

Rais Magufuli amteua Waziri Mkuu Mstaafu Pinda

26 May 2016 | Tanzania

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Waziri Mkuu Mstaafu Mheshimiwa Mizengo Peter Pinda kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT).

Mheshimiwa Mizengo Peter Pinda anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Dkt. Asha-Rose Mtengeti Migiro ambaye ameteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza.

Taarifa iliyotolewa  tarehe 25 Mei, 2016 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Mheshimiwa Pinda unaanza mara moja.

 

Gerson Msigwa

Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU

Dar es salaam

25 Mei, 2016

 

Ad