Home » Tanzania » Rais Magufuli amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Jiji la Dar es salaam Bw. Wilson Kabwe

Rais Magufuli amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Jiji la Dar es salaam Bw. Wilson Kabwe

19 April 2016 | Tanzania

Rais Magufuli amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Jiji la Dar es salaam Bw. Wilson Kabwe na kuagiza vyombo vinavyohusika kufanya uchunguzi dhidi ya tuhuma zinazomkabili za kusaini mikataba iliyosababisha serikali kupoteza mapato.

Dkt. Magufuli ametangaza uamuzi huo wakati akitoa hotuba ya ufunguzi wa daraja la Kigamboni, baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Bw. Paul Makonda kumueleza kuwa amebaini upotevu wa shilingi Bilioni 3 uliotokana na Mkurugenzi wa Jiji la Dar es salaam Bw. Wilson Kabwe kusaini mikataba ya ukusanyaji mapato ya Kituo Kikuu cha Mabasi Ubungo kwa kutumia sheria iliyopitwa na wakati, na pia ukusanyaji wa tozo za uegeshaji wa magari ndani ya Jiji.

 

Ad