Home » Tanzania » Rais Dr Magufuli ameteua watano leo

Rais Dr Magufuli ameteua watano leo

18 November 2016 | Tanzania

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 18 Novemba, 2016 amemteua aliyekuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera.

 

Uteuzi wa Bw. Diwani Athuman unaanza mara moja.

Wakati huo huo, Rais Magufuli amefanya uteuzi wa Wenyeviti wa Bodi katika taasisi tano za Serikali kama ifuatavyo.

Kwanza, Rais Magufuli amemteua Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA)

Uteuzi huu umeanza tarehe 16 Novemba, 2016.

Pili, Rais Magufuli

i - amemteua kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na

ii - amemteua kuwa Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Uteuzi huu umeanza tarehe 17 Novemba, 2016

Tatu, Rais Magufuli amemteua kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Uhandisi na Usanifu Mitambo (TEMDO).

Uteuzi huu umeanza tarehe 16 Novemba, 2016.

Nne, Rais Magufuli amemteua kuwa mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Fidia ya Ardhi.

Uteuzi huu umeanza tarehe 17 Novemba, 2016.

Tano, Rais Magufuli amemteua kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wakurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Viuatilifu vya Kitropiki Tanzania (TPRI)

Uteuzi huu umeanza tarehe 17 Novemba, 2016.

 

 

Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Dar es Salaam

18 Novemba, 2016

 

Ad