Home » Tanzania » Rais Dkt.Magufuli amemteua Bw. Gerson J. Mdemu kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali

Rais Dkt.Magufuli amemteua Bw. Gerson J. Mdemu kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali

24 May 2016 | Tanzania

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Bw. Gerson J. Mdemu kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Kabla ya Uteuzi huo, Bw. Gerson J. Mdemu alikuwa Karani wa Baraza la Mawaziri (Cabinet Clerk).

Bw. Mdemu anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Tulia Ackson ambaye amechuguliwa kuwa Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Wakati huo huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Profesa Longinus Rutasitara kuwa Mshauri wa Rais, masuala ya uchumi.

Kabla ya uteuzi huo Profesa Longinus Rutasitara alikuwa Mhadhiri wa Uchumi katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi leo tarehe 23 Mei, 2016 imeeleza kuwa uteuzi huu unaanza mara moja.

 

Gerson Msigwa

Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU

Dar es salaam

23 Mei, 2016

 

Ad