Home » Tanzania » Rais Dkt. Magufuli amemteua Mhandisi Paskasi Muragili kuwa Mkurugenzi Mkuu (CDA).

Rais Dkt. Magufuli amemteua Mhandisi Paskasi Muragili kuwa Mkurugenzi Mkuu (CDA).

20 April 2016 | Tanzania

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Mhandisi Paskasi Muragili kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu Dodoma (CDA).

Taarifa iliyotolewa leo tarehe 20 Aprili, 2016 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Mhandisi Paskasi Muragili umeanzia tarehe 17 Februari, 2016.

Kabla ya Uteuzi huo Mhandisi Paskasi Muragili alikuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu Dodoma (CDA), nafasi aliyoichukua kuanzia mwaka 2012.

 

Gerson Msigwa

Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU

Dar es salaam

20 Aprili, 2016

 

Ad