Home » Tanzania » Rais Dkt. Magufuli afanya uteuzi wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIDA

Rais Dkt. Magufuli afanya uteuzi wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIDA

16 February 2016 | Tanzania

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Modestus Francis Kipilimba kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA). Kabla ya Uteuzi huu Dkt. Kipilimba alikuwa Mkurugenzi wa Menejimenti ya Udhibiti (Director of Risk Management) katika Benki Kuu ya Tanzania. Dkt. Kipilimba anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Dikson Maimu ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.

Uteuzi huo utaanza tarehe 15 Februari, 2016

Ad