Home » Tanzania » Rais Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Samuel M. Nyantahe

Rais Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Samuel M. Nyantahe

25 July 2016 | Tanzania

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Samuel M. Nyantahe kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC).

Taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa Uteuzi huu umeanza tarehe 20 Julai, 2016.

Kabla ya uteuzi huo Dkt. Samuel M. Nyantahe alikuwa Mwenyekiti wa Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania (CTI).

Dkt. Samuel M. Nyantahe anachukuwa nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Chrisant Majiyatanga Mzindakaya ambaye amejiuzulu wadhifa huo.

 

Gerson Msigwa

Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU

Dodoma

25 Julai, 2016

 

Ad