Home » Tanzania » Marekebisho madogo katika majina yaliyopo kwenye orodha ya wakurugenzi

Marekebisho madogo katika majina yaliyopo kwenye orodha ya wakurugenzi

07 July 2016 | Tanzania

Tunapenda kufanya marekebisho madogo katika majina yaliyopo kwenye orodha ya wakurugenzi wa Halmashauri za Majiji, Manispaa, Miji na Wilaya ambapo

- Dkt. Leonard Moses Massale ametangazwa kuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma.

Jina hilo limeingizwa katika Orodha ya Wakurugenzi wa halmashauri kwa makosa, na kwa sababu hiyo Dkt. Leonard Moses Massale anaendelea kuwa Mkuu wa wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza.

Kufuatia marekebisho hayo, uteuzi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma utatangazwa baadaye.

 

Gerson Msigwa

Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU

Dar es salaam

07 Julai, 2016

Ad