Home » Tanzania » Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Amuwakilisha Rais UNIDO

Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Amuwakilisha Rais UNIDO

01 February 2016 | Tanzania

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Ujumbe wa Shirika la Maendeleo la Viwanda la Umoja wa Mataifa lenye Makao Makuu yake Nchini Vienna Austria uliongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo Bw. Li Yong, Januari 31,2016 kwenye Ofisi za Umoja wa Afrika (AU) Addis Ababa,

 

katika mazungumzo yao Viongozi hao walizungumzia juu ya kuendeleza ushirikiano kwenye maendeleo ya Viwanda utakaotolewa na UNIDO kwa Serikali ya Tanzania ili kuifanya Tanzania iwe Nchi ya Viwanda kuanzia mwaka 2015/2020, ambapo Mkurugenzi huyo ameahidi kuitembelea Tanzania wakati wowote kuanzia sasa. Makamu wa Rais yupo Nchini Addis Ababa Ethiopia kumuwakilisha Rais John Magufuli kwenye mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika unaojadili kuhusu masuala ya Usalama Barani Afrika.

Ad