Home » Tanzania » Makamu wa Rais Bi. Samia Suluhu atoa saa 24

Makamu wa Rais Bi. Samia Suluhu atoa saa 24

12 May 2016 | Tanzania
Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan ametoa masaa 24 kwa Mkuu wa Mkoa na uongozi wa jeshi la polisi na vyombo vingine  kuwasaka wauwaji hao popote walipo  na kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria.
 
Mhe. Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan, ametembelea Wilaya ya Sengerema kata ya Sima baada ya usiku wa kuamkia jana kutokea mauwaji ya kinyama kwa kuuwawa  watu saba wa familia moja.
 
Watu hao walio uwawa ni Mama na watoto sita.
 
Mauaji hayo ya kukatwa na mapanga na kupoteza familia  nzima yamekemewa na Mhe.
Mhe. Makamu wa Rais ameuagiza uongozi wa Mkoa wa Mwanza kusimamia shughuli zote za mazishi na gharama zake.
 
Mhe. Makamu wa Rais ametokea Mkoani Geita kwenye sherehe za siku ya Wauguzi Duniani na anarejea Mwanza kuendelea na shughuli za Serikali.
Ad