Home » Tanzania » Kupatwa Kwa Jua September 1, 2016 TUKIO LA KIHISTORIA

Kupatwa Kwa Jua September 1, 2016 TUKIO LA KIHISTORIA

29 August 2016 | Tanzania

Kupatwa huko kwa jua kutaanza kwenye bahari ya Atlantic, kutaenda Gabon, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Tanzania, Msumbiji na Madagascar na kisha kwenye bahari ya Hindi.

Wataalam wanadai kuwa Tanzania ndio itakuwa sehemu ambayo kupatwa huko kwa jua kutaonekana vyema zaidi na kuvutia watalii wengi kutokana na kile mtandao wa Independent wa Uingereza unasema ni “dependable weather, invariably clear “big skies”, abundant wildlife and peaceful reputation make it a top tourist destination.”

Maeneo yatakayoona vizuri tukio zima litakalochukua dakika tatu hadi sita ni kwenye maeneo ya Mbeya na Tunduru. Maeneo mengine ya Tanzania yatashuhudia tukio nusu.

Tayari makampuni ya safaris yameshapanga ratiba ya safari za kuja kwenye tukio hilo linalotokea kwa nadra sana.

Ad