Home » Tanzania » Flyover TAZARA Yaanza kujengwa, kukamilika Oktoba mwaka 2018.

Flyover TAZARA Yaanza kujengwa, kukamilika Oktoba mwaka 2018.

28 April 2016 | Tanzania

Ujenzi wa barabara za juu (fly over ) katika makutano ya barabara ya Nyerere na Mandela eneo la Tazara jijini Dar es salaam na utaghalimu kiasi cha shilingi bilioni 100 za Kitanzania.

Akizungumza katika sherehe za uwekaji jiwe la msingi Rais Dk.Magufuli amesema mradi huo utakapokamilika utasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza tatizo la msongamano wa magari katika jiji la Dar es salaam, ambao umekuwa ukipoteza fedha nyingi huku akitolea mfano tafiti ambazo zilifanywa mwaka 2013 ambazo zilionyesha zaidi ya shilingi bilioni 411.3 zilipotea kutokana na msongamano wa magari katika jiji la Dar es salaam.

Dk.Magufuli amesema serikali inaendelea na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo kujenga barabara itakayoanzia kigammboni mpaka chalinze ikiwa na barabara za juu 5 pamoja na ujenzi wa reli yenye standard geji ambayo itaanzia bandarini mpaka ruvu , ambapo magali ya mizigo yatakapokuwa yakichukulia mizino ili kupunguza msongamano.

Dk Magufuli amezungumzia pia kuhusiana na kucheleweshwa kwa mradi wa magari yaendayo haraka BRT ambapo amesema uko kwenye hatua za mwisho huku akidai kuwa kuna baadhi ya watu walitaka kufanya ujanja kuhusiana na mradi huo .

 

Ad