Home » Tanzania » Daladala kupisha DART kabla ya Mei 10,

Daladala kupisha DART kabla ya Mei 10,

05 May 2016 | Tanzania

Daladala zinazofanya safari zake katikati ya jiji zimetakiwa  kuondoka   ifikapo MeiHayo yameelezwa leo na Msemaji wa Mradi wa Mabasi yaendayo kasi (Dart),  ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Mabasi Mkoa wa Dar  es Salaam (Darcoboa), Sabri Mabrouk. Amelisema tayari wamiliki wote wa mabasi walishalipwa fidia ya kubadili njia.

 

“Wamiliki wote wa mabasi wameshalipwa fedha zao tangu Desemba mwaka jana, hakuna anayedai na tumewapa siku saba kuondoka barabara kabla ya Mei 10,” 

 

Mradi wa Dart unatarajia kuanza rasmi Mei 10, mwaka huu na tayari mabasi hayo yameshaanza kufanya majaribio katika njia mbali mbali katikati ya jiji.

Changamoto kubwa ikidaiwa na waendesha pikipiki, raia na daladala kupita kwenye njia hiyo ya mradi na kusababisha msongamano wa magari kitendo ambacho kinalazimu mabasi hayo nayo kujikuta yakikaa foleni. 

Ad