Home » Tanzania » Chama cha wananchi hakitoshirikia katika uchaguzi wa marudio

Chama cha wananchi hakitoshirikia katika uchaguzi wa marudio

28 January 2016 | Tanzania

Chama cha wananchi kimesema hakitoshirikia katika uchaguzi wa marudio  wa Visiwani Zanzibar uliopangwa kufanyika tarehe 20 marchi ya mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari muda mchache baada ya kumalizika kwa kikao cha Dharura cha baraza kuu la uongozi la Taifa,jijini Dar es Salaam,

Kaimu mwenyekiti wa Taifa CUF,Bwana Twaha Taslima, amesema wamefikia uwamuzi huo kutokana na uchaguzi huo kuwa ni batili

Aidha Bwana Twaha ameleza sababu ya kutoshiriki kwa katika uchaguzi huu unafatia Uhalali wa Mwenyekiti wa Tume Uchaguzi bwana Jecha Salum Jecha na kwenda kinyume na kikatiba na kisheria ya uchaguzi wa Zanzibar

Baraza hilo limetoa wito kwa jumuiya ya kimtaifa na hasa taasis zinazozimamia haki za bindamu na zinapambana na makosa ya jinai kimatifa kuchukua hatua dhidi ya kauli na matendo ya uhalifu,na uvunjwaji wa haki za bindamu na ubaguzi ambao umekuwa ukifanya dhidi ya wananchi wa Zanzibar

Ad