Home » Tanzania » Bw. Ally Salum Hapi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni

Bw. Ally Salum Hapi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni

19 April 2016 | Tanzania

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Bw. Ally Salum Hapi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mkoani Dar es salaam.

Bw. Ally Salum Hapi anachukua nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Bw. Paul Makonda ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam.

Uteuzi wa Bwana Ally Salum Hapi umeanza tarehe 18 Aprili, 2016.

 

Gerson Msigwa

Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU

Dar es salaam

18 Aprili, 2016

 

Ad