Home » Tanzania » AUDIO - Chama kipya cha CM-Tanzania chapata usajili wa muda

AUDIO - Chama kipya cha CM-Tanzania chapata usajili wa muda

04 February 2016 | Tanzania

Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi amekisajili chama kipya cha siasa nchini cha Maadili na Uwajibikaji (CM-TANZANIA) na kuwaasa viongozi wake kutekeleza wajibu wao katika kuleta maendeleo ya taifa kwani siasa sio chuki wala uhasama.

Akiongea katika makabidhiano ya cheti cha usajili leo, Jaji Mutungi amevitaka Vyama vya siasa nchini kufanya siasa na sio uanaharakati kwani kwa kufanya hivyo malengo yao yatatimia na kuifanya Tanzania kuwa na amani.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha Maadili na Uwajibikaji (CM-TANZANIA) Bwana Laban Nkembo amesema kuwa, chama hicho kimeanzishwa kwa lengo la kuiweka Tanzania kimaadili na uwajibikaji kwa kuwa kinabeba mambo makubwa mawili yakiwemo Amani na Upendo.

Ameongeza kuwa, chama chao sio cha upinzani na kinaheshimu chama kilichopo madarakani hivyo, kinaahidi kushirikiana na chama tawala kuenzi mazuri yanayofanywa na chama hicho.

CM-Tanzania ni chama cha 23 kupokea usajili baada ya vyama vingine vya siasa 22 vyenye usajili wa kudumu.
 
MSIKILIZE MWENYEKITI WA CAHMA HICHO
Ad