Home » Afrika » Serikali ya Burundi kujiondoa ICC

Serikali ya Burundi kujiondoa ICC

12 October 2016 | Afrika

Serikali ya Burundi imewapiga marufuku wataalamu watatu wa Umoja wa Mataifa baada ya kuchapisha ripoti iliyoituhumu serikali kwa ukiukaji wa haki za kibinadamu.

Ripoti iliyotolewa na wachunguzi hao ilibainisha maelfu ya watu kuteswa, kunyanyaswa kingono au kutoweka wakati wa machafuko ya kisiasa yaliyotokea tangu Aprili mwaka jana.

Watalaamu hao walitahadharish akatika ripoti yao juu ya uwezekano wa kutokea mauaji ya halaiki kutokana na kuongezeka kwa machafuko.

Hayo yanajiri wakati huu Burundi pia ikiwa imetangaza mpango wa kujiondoa katika mkataba wa Roma unaotambua Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita ICC.

Ad