Home » Afrika » Moise Katumbi Chapwe kuchunguzwa

Moise Katumbi Chapwe kuchunguzwa

05 May 2016 | Afrika

Siku moja baada ya Gavana wa zamani wa Jimbo la Katanga nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Moise Katumbi Chapwe kutangaza nia yake ya kuwania urais mwezi Novemba kupitia muungano wa vyma vya upinzani, serikali nchini humo imeamuru uchunguzi kufanyika dhidi ya mwanasiasa huyo kutumia mamluki kutoka Marekani kumlinda.

Hata hivyo, madai haya yamekanushwa na Katumbi ambaye amesema ni ya uongo na hawezi kutumia silaha kuingia madarakani.

Nchini DRC, kwa sasa kinachojadiliwa na wengi hasa wakaazi wa jimbo la Katanga ni uamuzi wa Katumbi kuamua kuwania urais.

Ad