Home » Nje Ya Afrika » Watu 15 wafariki baada ya gari lililobebea gesi kulipuka nchini Pakistan

Watu 15 wafariki baada ya gari lililobebea gesi kulipuka nchini Pakistan

10 February 2016 | Nje ya Afrika

Takriban watu 15 wakiwemo watoto 10 wa shule wamefariki na wengine wengi kujeruhiwa, kufuatia gari la kubebea gesi kulipuka leo asubuhi baada ya kugongana na gari jingine mashariki mwa Pakistan.

Ajali hiyo ilisababisha moto mkubwa, uliofunika gari mbili zilizokuwa zikipita pamoja na riksho mbili zilizokuwa zikibeba watoto wanaokwenda shule. Majeruhi wakiwemo wanawake na watoto wa shule wamepelekwa hospitali, na baadhi yao wako katika hali mahututi.

Ripoti rasmi ya chanzo cha ajali hiyo itatolewa baada ya polisi kumaliza uchunguzi. Hata hivyo, mashuhuda walisema dereva alishindwa kudhibiti gari lake na kuligonga gari jingine kutokana na ukungu mzito.

Ad