Home » Nje Ya Afrika » WAANDISHI WA AFRIKA JIFUNZENI KUFICHA MABAYA YENU, TANGAZENI MAZURI KWANI YANAYOENDELEA ULAYA NI HATARI MNO

WAANDISHI WA AFRIKA JIFUNZENI KUFICHA MABAYA YENU, TANGAZENI MAZURI KWANI YANAYOENDELEA ULAYA NI HATARI MNO

27 December 2018 | Nje ya Afrika

Usiyoyajua kuhusu maandamano ya Ufaransa

Prof. Dr. Kudret BÜLBÜL

Nchini Ufaransa na katika baadhi ya mataifa ya ulaya kwa mawiki kadhaa sasa tumeshuhudia maandamano makubwa ambayo waliyaita “vizibao vya njano”, tumeshuhudia moto ukiwaka. Vifo pia vilikuwako katika matukio hayo, Nchini Ufaransa mwishoni mwa wiki iliyopita peke yake kwa mujibu wa taarifa rasmi kutoka serikalini mamia ya waandamanaji walijeruhiwa huku maelfu ya waandamanaji wakitiwa nguvuni.

Je nini kimeisibu Ulaya? 

Wananchi wa Ulaya wamejifungia na wanaishi kama vile ilivyokuwa kabla ya vita kuu ya 2 ya dunia.

Sababu zinazopelekea upinzani unaoonyeshwa na jamii za ulaya dhidi ya wahamiaji, waislamu, wayahudi na wageni kutoka nchi nyingine. Chanzo cha matatizo sio wahamiaji bali ni jamii zenyewe za Ulaya. Tatizo ni kuhusu mustakabali wa Ulaya, kama tunavyoona kinachojiri hivi sasa. “

Je Ulaya itajenga maadili kupitia Umoja wa Ulaya? Au wataandelea kutumia unazi na ubeberu waliorithi kutoka zama za kale? ”

Kuhusiana na hili tulisisitiza kwamba kama  makundi ya watetezi wa uhuru katika jamii za Ulaya yasipopaza sauti zao kulisema hili , itafikia muda watakuwa wamechelewa na wasiweze kufanya chochote.

Matukio ya nchini Ufaransa

Maandamano ya nchini ufaransa ya hivi karibuni unaweza kusema yanatokana na jamii hiyo kujifungia, chuki na ubaguzi kuonekana kitu cha kawaida, na jamii hizo kujali maslahi yao zaidi kuliko kitu chochote.

Matukio ya vizibao vya njano hayakusababishwa na wahamiaji, bali yanatokana na jamii hizo kushindwa kuendana na kasi ya utandawazi, yalitokana na mkwamo wa uchumi, yalitokana na Ufaransa kushindwa kudumisha ustawi wa jamii uliokuwako zamani.

Matukio yanayoendelea duniani hivi sasa pamoja na nguvu nyingine za kiuchumi zinazoibuka, vinaifanya Ufaransa na mataifa mengine ya Ulaya kushindwa kudumisha ustawi wa jamii na kuleta maendeleo.

Matukio na vyombo vya habari

Katika matukio yaliyotokea İstanbul kwenye eneo la Gezi, karibu vyombo vya habari vya dunia nzima viliweka kambi pale walirusha matangazo ya moja kwa moja kwa masaa bila kukoma. Hatuwezi kusahau jinsi vilivyowafanya waandamanaji kuwa mashujaa

Bado yule binti aliyekuwa na kilemba chekundu na alama ya mwanaume aliyesimama vipo kwenye akili zetu. Vyombo vya habari vililikuza tukio vilionyesha kwamba Uturuki na hasa polisi ni wavunjifu wakubwa wa haki za binadamu

Tukirudi katika matukio ya Paris, vyombo vya habari vya Ulimwengu vimeyapa nafasi ndogo sana. Vyombo hivyo havikuripoti vya kutosha nguvu kubwa iliyotumiwa na polisi dhidi wanafunzi wa sekondari walioshiriki maandamano hayo. Havikuonyesha uvunjifu huu wa haki za binadamu.

Je vizibao vya njano wanataka nini?

Vizibao vya njano ni kama vile ilani ya uchaguzi ya  chama cha siasa, wamefahamisha mambo 42 ambayo ni kero, Kero zao ni zaidi ya bei kubwa ya mafuta . Kero nyingine za waandamanaji hao wa vizibao vya njano ni pamoja na gharama kubwa ya maisha, tozo kubwa la kodi, mazingira mabovu ya kufanya kazi, hatua dhidi ya wahamiaji, kanuni za uchaguzi.

 

 Waa ndamanaji hao walizitaja kero mbalimbali katika sekta tofauti kuanzia siasa, jamii, uongozi kiasi kwamba unaweza kufananisha mahitaji yao na ilani ya uchaguzi wa chama cha siasa, lilikuwapo pia hitajio la Kuongeza muda wa uraisi mpaka kufikia miaka 7.

Kuipindua serikali kupitia mtaa na sio sanduku la kura...

Bila shaka demokrasia ni njia bora. Katika jamii za kidemokrasia aina yeyote ya mahitaji inaweza kuwasilishwa. Kwa ajili hiyo uhuru wa kufanya mikutano na uhuru wa kundamana ni vitu vya msingi sana kwa nchi inayofuaata mfumo wa kidemokrasia. Kwa waliopo madarakani kukubaliana na hili mara nyingine kunakuwa ugumu. Katika jamii za kidemokrasia kutumia nguzu kubwa dhidi ya waandamanaji ni kosa la jinai kwani ni uvunjifu wa haki za msinigi za binadamu.

Pamoja na  yote hayo katika jamii za kidemokrasia njia pekee ya kubadilisha utawala inafahamika. Katika demokrasia njia ya kuwatoa watawala wasiohitajika kwenye madarakani sio kuandamana bali ni kutumia sanduku la kura. Lakini watu hutumia maandamano na vurugu, kuharibu maeneo ya kazi, kuchoma moto, kubomoa, kuvunja, kushambulia watu wasio na hatia na mambo mengine kama hayo ili kulazimisha mabadiliko katika utawala. Kutumia njia isiyokuwa sanduku la kura kuondoa utawala ulioko madarakani, kama vile vurugu na maandamano ya mitaani huleta machafuko na ufashisti. Katika bara ya Ulaya ni bora apatikane kiongozi fashisti ambaye amechaguliwa na walio wengi kuliko  mitaa kukumbwa na vurugu na uharibifu wa maandamano, ambayo ni vigumu  kutabiri mwisho wake.

Mapinduzi ya Ufaransa urithi kwa Utu

Kwa bahati mbaya nchi ya Ufaransa katika matokeo ya harakati za kimtaa ni nchi yenye kumbukumbu ya machungu.  Inafahamika mapinduzi ya Ufaransa ambayo yalianza na mawazo kama “Uhuru, Usawa na Undugu” yaliishia katika umwagaji damu mkubwa. Lakini bado tunaona watu wanaojiita wazawa katika maeneo mbalimbali wanakuja na aina hio hio ya mapinduzi na wanaendelea kuivuruga dunia. Shauku ya kupata uhuru inapelekea kuacha mataifa yamegawanyika na kuparanganyika.

Vivyo hivyo, aina ya elimu ya Kifaransa imewasilisha kwa ubinadamu  kielelezo cha kutumia akili na hutoa mtazamo wa juu wa mapambano unaozingatia kila kitu ambacho hakionekani kuwa kizuri, wakati wa kuadhimisha mtazamo wake. Katika historia ya binadamu vita nyingi zilizosababisha umwagaji wa damu mkubwa , vifo vingi na mauaji ya kimbari vilitokea wakati ustaarabu ukiwa umeshamiri, sio vigumu kutabiri kitachotokea pale binadamu watakapo achana na mambo ya kimsingi yanayowawekea mipaka kama  utamaduni,maadili, dini na  Mungu.

Leo hii kila mtu ana haki ya kuwa na wasiwasi na yanayoendelea katika kutengeneza binadamu wa bandia kwa kubadilisha vinasaba. Kwani hili linaweza kupelekea mwisho binadamu duniani.

Nafasi ya ustaarabu wa kifaransa katika dunia tuliopo haiwezi kupingwa, Kama ikitumika sawasawa suala la kutengeneza binadamu wa bandia halitakuwa na nafasi katika akili ya binadamu.

Harakati za kimtaa au mapinduzi ya serikali kwa njia ya maandamano yanafahamika kwa matokeo yalisababisha umwagaji mkubwa wa damu. Haya yamesibitishwa katika kitabu kilichoandikwa na Edmund Burke wakati wa mapinduzi, kilichoitwa kumbukumbu ya mpinduzi ya Ufaransa “Reflection on French Revolution”. Kama jinsi Berat Özipek alivyofafanua,Ni kwamba Burrke aliandika kabla Jakobbenler hajaingia madarakani, kabla misingi ya uhuru, usawa na undugu haijatumiwa kupelekea damu nyingi kumwagika, kabla ya mfalme, malkia,viongozi wa dini na maelfu ya watu wa kawaida hawajahukumiwa kunyongwa. Je Robespierre hakuwanyonga wapinzani wake kitu ambacho kilipelekea Robespierre naye kunyongwa ?.

Kwa mara nyingine tena inaonekana aina mpya ya vurugu zinaenea duniani zikitokea Ufaransa. Vurugu hizi zinaweza kusabibisha madhara makubwa zaidi kwa mataifa mengine ya magharibi.

Ndiyo ingawa matukio ya aina hiyo yalipotokea Uturuki au katika jamii zisizokuwa za magharibi yalikuzwa, na jamii kushushwa pamoja na kuonekana  hazijastaaribika.

Hatuwezi kusema kwa kuwa wao walifanya vile basi na sisi tufanye hivi kwa kuwa Ufaransa na Magharibi sio waalimu wetu .

Kwetu katika hali zote hata kama ikiwa zinawahusu mabeberu, na mataifa ya magharibi yatupasa kuwa waadilifu, Inatupasa kufikiria wanajamii wa magharibi na utu kwa ujumla

Ufafanuzi wa Prof. Dr. Kudret BÜLBÜLmkuu wa kitivo cha elimu ya siasa chuo kikuu cha Ankara Yıldırım Beyazıt,

WAANDISHI WA AFRIKA JIFUNZENI KUFICHA YENU YANAYOENDELEA ULAYA NI HATARI MNO  

Maandamano yaendelea...

Maandamano yaendelea nchini Ufaransa

Jiji la Paris  linakabiliwa na  ghasia kutokana na maandamno yanayoendelea  kama alivyoshuhudia rais Macron... ni wimbi la nne la maandamano kuhusu rais Macron akitazamwa ni upi uamuzi utakoachukuliwa, kama itakuwa  kutangazwa kwa hali ya  dharura.  Uamuzi utakochukuliwa unasubiriwa kwa  hamu kubwa na waandamanaji  Waandamana kwa mara nyingine wameandamana kupinga kupanda kwa bei za mafuta. 

Watu zaidi ya 136 000 wanaandamana kupinga bei  za mafuta kupanda, Jiji la Paris laathirika  kwa moto  magari zaidi ya 100  yameteketea, majumba 6, vituo vya mabasi pia vimeteketea kwa moto  Ghasia zimezidi  pindi siku zinavyosomba mbele   Jeshi la Polisi la kutuliza ghasia  limefahamisha , kuwakamata watu zaidi ya 412 katika maandamano  miongoni mwao 33 wakiwa na umri wa chini ya miaka 18  na wengine zaidi ya 100 wamewekwa rumande.

Waziri wa sheria Nicole Belloubet asema kwamba watu  waliokamatwa watafikishwa mahakamani  kujibu tuhuma zinazowakabili  Watu 263 wamejeruhiwa  katika maandamano hayo.

Rais Macron  baada ya mkutano wa G20 Argentina alikutana na mawaziri wake katika  mkutano  na kuonesha msimamo wake kuwa ni ule ule Rais Emmanuel Macron ametolea wito viongozi wote wa upinzani kukutana. 

Kunatarajiwa kufanyika mkutano kati ya Macron na wawakilishi wa vyama vya upinzani.    

Waziri Edouard Philipp anatarajiwa kukutana kwa mara nyingine   na wawakilishi wa waandamanaji  licha ya ahadi za mikutano   maandamano yanaonekana kuzidi kupamba moto waandamanaji wakisema kuwa  wataendelea na maandamano  Jumamosi  ijayo iwapo maombi yao hayatotekelezwa .

Waandamanaji wapo tayari kuendelea na maandamano Maandamano sio tu Paris, maandamano pia yanafanyika katika miji mingine kama Strasbourg, Lille na Marseille  wafanyakazi katika mashirika ya kutoa huduma ya kwanza wameandamana  kwa kukutana  katika mnara wa Concord  tangu majira ya asubuhi.  

Waandamanaji wanadai  haki zao za msingi  za kikatiba  na sheria katika maandamano hayo.

Ad