Home » Nje Ya Afrika » Trump na Clinton waongoza vyama vyao

Trump na Clinton waongoza vyama vyao

02 March 2016 | Nje ya Afrika

Wagombea wote wawili wameshinda majimbo ya Alabama, Georgia, Tennessee na Virginia.

Bw Trump hata hivyo ameshindwa na Seneta Ted Cruz majimbo ya Texas na Oklahoma.

Mgombea wa Democratic Bernie Sanders naye ameshinda kwake nyumbani katika jimbo la Vermont na pia katika jimbo la Oklahoma.

Mchujo wa Jumanne Kuu hushuhudia majimbo 11 yakifanya mchujo kwa pamoja huku maandalizi ya uchaguzi mkuu tarehe 8 Novemba yakiendelea kushika kasi.

Bi Clinton pia ameshinda Arkansas na Texas, naye Bw Trump akashinda Massachusetts.

Utafiti wa maoni ya paada ya kura unaonyesha Trump na gavana wa Ohio John Kasich wakikabiliana vikali katika mchujo wa chama cha Republican jimbo la Vermont.

Bi Clinton na Bw Sanders pia wanakabiliana vikali katika jimbo la Massachusetts, kaskazini mashariki mwa Marekani.

Ad