Home » Nje Ya Afrika » Sterling Pound yaporomoka kiwango kikubwa zaidi

Sterling Pound yaporomoka kiwango kikubwa zaidi

24 June 2016 | Nje ya Afrika

Thamani ya sarafu ya Uingereza, Sterling pound imeshuka kwa kiwango kikubwa mno kuwahi kutokea katika kipindi cha miaka 30 iliyopita.

Wafanyibiashara wamepandwa na ghadhabu kubwa kutokana na matokeo ya kura ya maoni nchini Uingereza ambayo imeonesha wazi kuwa asilimia 52% ya Waingereza wangependa taifa hilo lijiondoe katika muungano wa EU.

Katika saa ya kwanza ya kuhesabu kura hiyo ya maoni, pauni ya Uingereza ilipanda na kuishinda dola ya Marekani, lakini kwa sasa imeshuka baada ya matokeo ya kura hiyo kuanza kuonyesha dalili ya Uingereza kujiondoa kutoka katika muungano wa mataifa ya bara Ulaya.

Wafanyibiashara wanasema kuwa hawajawahi kushuhudia mabadiliko makubwa ya kifedha kiasi hicho tangu wakati wa mdororo wa uchumi mwaka 2008.

Ad