Home » Nje Ya Afrika » Rais Obama kufanya ziara yake ya kwanza katika msikiti

Rais Obama kufanya ziara yake ya kwanza katika msikiti

03 February 2016 | Nje ya Afrika

Rais wa Marekani Barack Obama anatarajiwa kufanya ziara yake ya kwanza katika msikiti mjini Baltimore Marekani, hatua ambayo inachukuliwa kama  ishara kuwa serikali ya Marekani haina ubaya wowote na dini ya kiisilamu.

Msemaji wake rais obama amefahamisha kuwa itakuwa ni ziara fupi, ambako atakutana na viongozi wa jamii ya Waislamu na kutoa hotuba.
Wachambuzi wa siasa mjini Washington wamesema kitendo cha Obama kuonyesha dhamira yake kuingia msikitini ni kupinga matamshi yasiyofaa ya wagombea wa chama cha Republican dhidi ya Waisilamu, lakini pia ni njia ya kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya m,arekani na mataifa ya kiisilamu .

Hii si mara ya kwanza rais Obama anatembelea waisilamu, Aliwahi kutembelea misikiti nchini Malaysia , Indonesia na Misri akiwa rais, lakini bado hajawahi kutembelea msikiti nchini Marekani.

 

Ad