Home » Michezo » Bao la kwanza la Samatta akiichezea KRC Genk

Bao la kwanza la Samatta akiichezea KRC Genk

01 March 2016 | Michezo

KRC Genk imefanikiwa kuifunga Club Brugge mabao 3-2, lakini story kubwa ni kumshuhudia Mbwana Ally Samatta akifunga bao la tatu ambalo lilikuwa ni bao lake la kwanza tangu ajiunge na timu hiyo.

Ulikuwa ni mchezo wake wa nne akitokea benchi leo kwenye mchezo ambao Genk walikuwa wakihitaji pointi tatu muhimu huku wakihitaji kumaliza katika nafasi 6 za juu ili waweze kuingia kwenye play off. wamefanikiwa kupata ushindi huo  na kutengeneza mazingira mazuri ya kuweza kumaliza katika nafasi 6 za juu kwenye ligi.

Baada ya mchezo kumalizika, namna ambavyo amejisikia hasa baada ya kufunga bao la kwanza akiwa na klabu yake mpya ya Genk.

“Ni kitu ambacho nilikuwa nakiota, kila siku unapokuwa kwenye timu mpya watu wanaangalia action yako ya kwanza yaani umeanzaje kwenye timu mpya na ni kitu muhimu kuwa na confidence baada ya hapo inahitaji kuendeleza kwahiyo ndiyo chalenge ambayo imebaki kwangu mimi”, anasema Samatta ambaye ni nahodha wa kikosi cha Taifa Stars.

“Kwasababu kama mwanzo tayari umeshaonekana ni mzuri lakini ngumu ni kuendelea kuwa hivyo nafikiri ni changamoto kwangu na nitajitahidi niweze kushinda hiyo changamoto na niendelee kufunga magoli”.

Ad