Home » Burudani » BASATA wametoa ujumbe kuwataka LINO na kurudi mezani

BASATA wametoa ujumbe kuwataka LINO na kurudi mezani

05 February 2016 | Burudani

Baraza la sanaa Tanzania (BASATA) limefungua makucha na kuitaka kampuni ya LINO waandaaji wa mashindano ya Miss Tanzania kurudi mezani na kamati ya mashindano hayo ambayo ilijitoa wiki kadhaa nyuma kushiriki katika mashindano hayo ambayo awali yalikuwa yamefungiwa.

Basata  wametoa ujumbe kuwataka LINO na kurudi mezani na kuangalia namna bora ya kusonga mbele kwa kuweka mipaka ya utendaji kati yake na kamati hiyo.

"BASATA imeitaka kampuni ya LINO waandaaji wa Miss Tanzania kurudi mezani na kamati ya shindano kujadiliana namna bora ya kusonga mbele, Tumeiagiza LINO kuandaa MoU na kamati ya shindano la Miss Tanzania ili kuchora mipaka ya kiutendaji baina yao" Wamesema Basata.

Ikumbukwe kamati ya Miss Tanzania chini ya viongozi wake Mwenyekiti Juma Pinto, Jokate Mwengelo, na Gladys Shao ilitangaza maamuzi hayo ya kujitoa katika mashindano ya Miss Tanzania wiki kadhaa zilizopita na kusema wamefanya hivyo baada ya kupishana katika baadhi ya mambo ya kiutendaji ya kamati hiyo.