Home » Bunge » Kamati za Kudumu za Bunge zimeanza kukutana Mjini Dodoma

Kamati za Kudumu za Bunge zimeanza kukutana Mjini Dodoma

16 January 2017 | Bunge

Kamati za Kudumu za Bunge zimeanza kukutana Mjini Dodoma kutekeleza majukumu yake kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Sita wa Bunge uliopangwa kuanza tarehe 31 Januari 2017. Kufuatia ratiba hiyo ya shughuli za Kamati, Waheshimiwa Wabunge wote tayari  wamewasili Mjini Dodoma tayari kwa kuanza vikao vya Kamati.

Katika kipindi chote hiki cha vikao hivyo, shughuli zilizopangwa kutekelezwa na Kamati ni kama ifuatavyo:

a) ZIARA ZA UKAGUZI WA MIRADI YA MAENDELEO

Katika utekelezaji wake wa majukumu, Jumla ya Kamati 12 zitafanya ziara za kukagua miradi ya maendeleo katika maeneo mbalimbali nchini inayotekelezwa na Wizara/Idara zinazosimamiwa na Kamati husika. Ziara hizo zitafanyika kuanzia, Tarehe 17 hadi 21 Januari, 2017 kabla ya kuendelea na vikao tarehe 23 Januari, 2017 Mjini Dodoma.

b) KUPOKEA MAONI YA WADAU WA MISWADA MBALIMBALI

Kamati mbili (2) za Kisekta zitajadili Miswada Mitatu ya Sheria ambapo Kamati ya Katiba na Sheria itajadili Miswada miwili ambayo ni:

· Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali, Na. 4 wa Mwaka, 2016 [The Written Laws (Miscellaneous Amendments) Bill, 2016] na Muswada wa Sheria ya Huduma ya Msaada wa Kisheria wa Mwaka, 2016 (The Legal Aid Bill, 2016). Kamati hiyo itakuwa na vikao vya kupokea maoni ya wadau kuhusu Miswada hiyo siku ya tarehe 19 na 20 Januari, 2016 Katika ukumbi wa Serengeti ulipo katika Jengo la Hazina Ndogo Mjini Dodoma kuanzia saa tatu kamili (3:00) asubuhi hadi saa Tisa(9:000) Alasiri

· Kamati nyingine ni Kamati ya Huduma na Maendeleo ya Jamii ambayo itachambua Muswada wa Sheria ya Madaktari, Madaktari wa Meno na Wataalam wa Afya shirikishi wa Mwaka 2016 (The Medical, Dental and Allied Health Professionals Bill, 2016) na itakuwa na vikao vya kupokea maoni ya wadau kuhusu Muswada huo siku ya tarehe 18 Januari, 2017 Katika ukumbi ulipo Jengo la Utawala Annex kwenye Viwanja vya Bunge Mjini Dodoma kuanzia saa tatu kamili (3:00) asubuhi hadi saa Tisa (9:000) Alasiri.

Wadau wote katika Miswada tajwa hapo juu wanakaribishwa kufika mbele ya Kamati kutoa maoni yao katika tarehena muda uliotajwa.

c) KUPOKEA TAARIFA ZA KIUTENDAJI WA WIZARA

Aidha kuanzia tarehe 23 hadi 27Januari,2017, Kamati za kisekta zitaendelea kupokea Taarifa za kiutendaji wa Wizara zinazosimamiwa na Kamati hizo kwa mujibu wa Kifungu cha 7 (1) (c) na (d) cha Nyongeza ya Nane ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo Januari, 2016.Ratiba zoteza Shughuli za Kamati za Bunge ikiwa ni pamoja na maeneo ambayo kamati hizo zitafanya ziara, pamoja na Miswada itakayoshughulikiwa na Kamati katika kipindi hiki vinapatikana katika Tovuti ya Bunge ambayo ni