Home » Afrika » Zoezi la kuhesabu kura linaendelea nchini jamuhuri ya afrika ya kati

Zoezi la kuhesabu kura linaendelea nchini jamuhuri ya afrika ya kati

15 February 2016 | Afrika

Zoezi la kuhesabu kura linaendelea nchini jamuhuri ya afrika ya kati baada ya kukamilika kwa upigaji kura siku ya jumapili katika uchaguzi wa duru la pili ambao unatazamiwa huenda ukatamatisha uhasama na ghasia za kidini katika taifa hilo.

Kura zilipigwa chini ya ulinzi mkali huku waangalizi wa umoja wa mataifa wakisambazwa nchi nzima na kushuhudia uchaguzi ukitamatika kwa amani.

Zoezi hilo la kuhesabu kura lilianza jana jumapili katika madarasa ya shule zilizotengwa kuwa vituo vya kupigia kura nchini humo.

Ushindani mkali katika uchaguzi huo ni kati ya Mawaziri Wakuu wawili wa zamani Anicet Georges Dologuélé na Faustin Archange Touadéra,ambao wote wawili katika kampeni zao wameahidi kurejesha usalam ana kuinua hali ya uchumi katika taifa hilo linalokabiliwa na hali mbaya ya umasikini.

Ad