Home » Afrika » Watu wawili wameuawa baada ya kuteketezwa moto jijini Lusaka ZAMBIA

Watu wawili wameuawa baada ya kuteketezwa moto jijini Lusaka ZAMBIA

20 April 2016 | Afrika

Polisi nchini Zambia inasema watu wawili wameuawa baada ya kuteketezwa moto jijini Lusaka.

Kuanzia wiki hii, raia wa Zambia wamekuwa wakiwavamia raia wa kigeni hasa wale kutoka Rwanda kwa madai kuwa wamekuwa wakihusika na mauaji ya wazawa na kutumia sehemu za miili yao kwa sababu za kishirikina.

Ripoti zinasema raia saba wa Zambia wameuawa jijini Lusaka wiki hii na masikio, sehemu za siri na nyonyo za watu hao zikinyofolewa.

Maandamano yalishuhudiwa jijini Lusaka siku ya Jumatatu na maduka na makaazi ya raia wa kigeni hasa ya Wanyarwanda yakishambuliwa lakini leo Jumatano hali imekuwa tulivu.

Hali hii imezua hali ya wasiwasi kwa raia wa kigeni ncnini humo.

Mashambulizi kama haya yaliwahi kushuhudiwa nchini Afrika Kusini mwaka uliopita.

Ad