Home » Afrika » Watu wawili wamejeruhiwa baada ya ndege ya Somalia kutokea mlipuko

Watu wawili wamejeruhiwa baada ya ndege ya Somalia kutokea mlipuko

03 February 2016 | Afrika

Polisi nchini Somalia wamesema kuwa watu wawili wamejeruhiwa baada ya ndege waliyokuwa wanasafiria kushika moto, huku wengine zaidi ya hamsini wakiwa salama.

Maafisa wa usalama nchini humo wanasema ndege ya shirika linalofahamika kama Daallo Airlines, ililazimika kutua katika hali ya dharura punde baada ya rubani wa ndege hiyo Vladimir Vodopivec, mwenye umri wa miaka 64, kusikia kitu kama mlipuko wa bomu.

Kabla ya kuanza safari mafundi wa ndege hiyo ya abiria ambayo ilikuwa imeanza safari kutoka mogadishu kwenda Djibouti, wamesema hawakutambua kuwa ingetokea hitilafu yoyote ya kiufundi.

Hayo yanajiri wakati Watu kadhaa wanahofiwa kuuawa katika milipuko mitatu iliyotokea kwenye shule moja iliyo karibu na ikulu ya rais mjini Mogadishu, Somalia, mapema jana.

Mkuu wa wilaya ya Wardhhigley, Yassin Nor Isse amethibitisha kuwa makombora kadhaa yalirushwa karibu na ikulu ya rais, Villa Somalia, mjini Mogadishu. Ameongeza kuwa, taarifa za awali zinasema raia kadhaa wamepoteza maisha. Hadi sasa ni mtu moja aliyethibitishwa kupoteza maisha katika hujuma hiyo.

Ad