Home » Afrika » Watu 400 wameuawa nchini Ethiopia

Watu 400 wameuawa nchini Ethiopia

16 June 2016 | Afrika

Shirika la Kimataifa la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch linasema tangu mwezi Novemba mwaka uliopita, watu 400 wameuawa nchini Ethiopia.

Amnesty International inasema watu hao wameuawa mikononi mwa maafisa wa usalama nchini humo kwa kujaribu kuikosoa serikali ya Addis Ababa.

Hata hivyo, serikali imetupilia mbali ripoti hiyo na kusema haina ukweli wowote.

Ripoti hiyo inasema watu waliouawa ni kutoka jamii ya Oromo ambao wamekuwa wakiishtumu serikali kwa kuwa na mpango wa kupanua eneo la jiji la Addis Ababa na kuchukua mashamba yao.

Shirika hilo linasema limewahoji watu zaidi ya 100 ambao wamekiri kuwa wapendwa wao waliuawa na wengine kuteswa na maafisa wa usalama baada ya kuandamana kupinga mradi huo ambao hatimaye serikali ilitangaza kuachana nao mwezi Januari mwaka huu.

Msemaji wa serikali Getachew Reda amesema mara kwa mara Shirika hilo likitoa ripoti yoyote kuhusu Ethiopia, limekuwa likitoa ripoti za uongo.

Ad