Home » Afrika » Wapiganaji makundi ya kiislamu wameshambulia kambi nchi ya Mali

Wapiganaji makundi ya kiislamu wameshambulia kambi nchi ya Mali

12 February 2016 | Afrika

Wapiganaji wanaodaiwa kuwa ni kutoka makundi ya kiislamu wameshambulia kambi ya wanajeshi wa kulinda amani wa umoja wa mataifa kaskazini mwa nchi ya Mali kwenye mji wa Kidal, ambapo watu kadhaa wameripotiwa kufa na wengine kujeruhiwa, amesema msemaji wa kundi la vuguvugu la Azawadi.

Tume ya MINUSMA nchini humo bado haijatoa taarifa rasmi kuhusu idadi kamili ya watu waliouawa, ingawa msemaji wa tume hiyo, amethibitisha watu kadhaa kupoteza maisha kwenye shambulio hilo lililotekelezwa majira ya saa kumi na mbili asubuhi ya leo.

Kambi hiyo ya walinda amani kwenye mji wa Kidal, ilifunguliwa kwa lengo la kuimarisha usalama kwenye eneo la kaskazini mwa nchi hiyo, ambalo linaendelea kushuhudia matukoo ya hapa na pale ya wapiganaji wa kiislamu.

 

Ad