Home » Afrika » Wanajeshi walioasi kwenye jeshi la Sudan Kusini kwenye majadiliano na utawala wa Juba

Wanajeshi walioasi kwenye jeshi la Sudan Kusini kwenye majadiliano na utawala wa Juba

14 March 2016 | Afrika

Hatimaye wanajeshi walioasi kwenye jeshila Sudan Kusini na kwenda kupigana sambamba na aliyekuwa makamu wa rais Riek Machar, wamewasili mjini Juba wakimaliza miezi kadhaa ya majadiliano na utawala wa Juba.

Miongoni mwa waliowasili mjini Juba hapo jana ni pamoja na aliyekuwa jenerali wa jeshi la Sudan Kusini kabla ya kuasi, Jenerali, Gathoth Gatkuoth, james Malith Gatluak, Chuol Gakah na Gabriel Yoal Dok, mwenyekiti wa kabila la Nuer walioambatana na wapiganaji wao.

Haijafahamika bado, ikiwa baadhi ya viongozi wa juu wa waasi waliojisalimisha watapewa jukumu gani kwenye serikali ijayo, kwakuwa baadhi ya waliojisalimisha walikuwa wamejitenga na Riek Machar kwa lengo la kuendeleza vita ili kumuondoa madarakni rais Salva Kiir na kuhakikisha Riek Machar na ahusishwei kwenye serikali ijayo.

Mshauri wa rasi Kiir kuhusu masuala ya usalama, Tut Gatluak ambaye aliambatana na ujumbe huo mjini Juba, amepongeza hatua hii mpya na kusisitiza utayari wa Serikali kuhakikisha inamaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.

Ad