Home » Afrika » Upinzani nchini Niger umesema kuwa hautashiriki Duru ya pili

Upinzani nchini Niger umesema kuwa hautashiriki Duru ya pili

09 March 2016 | Afrika

Upinzani nchini Niger umesema kuwa hautashiriki Duru ya pili ya uchaguzi wa rais ambao umepangwa kufanyika tarehe 20 mwezi huu wa Marchi.

Uchaguzi huu utafanyika wakati Hama Amadou, hasimu wa Rais Mahamadou Issoufou wa Niger katika duru ya pili ya uchaguzi wa rais nchini humo, bado anaendelea kushikiliwa na vyombo vya dola licha ya kukaribia uchaguzi huo.

Serikali ya Niamey imetangaza kuwa, Amadou hatopewa fursa ya kushiriki katika kampeni za uchaguzi na kwamba ataendelea kusalia korokoroni hadi siku ya uchaguzi.

Ni hatua ambayo inakuja wakati upinzani kwa pamoja umesema pamoja na kufupishwa kwa muda wa kamepni wao wameamua kujiondoa.

Ad