Home » Afrika » Umoja wa Mataifa unachunguza Afrika ya Kati

Umoja wa Mataifa unachunguza Afrika ya Kati

17 February 2016 | Afrika

Umoja wa Mataifa unachunguza tuhuma mpya za vitendo vya udhalilishaji wa kingono vinavyofanywa na askari wake wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, tuhuma ambazo zitakuwa si za kwanza kuelekezwa kwa wanajeshi hao.

 

Msemaji wa umoja wa Mataifa, Farhan Haq, amesema kuwa tayari timu ya wachunguzi kutoka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, imeshatumwa nchini humo kuchunguza tuhuma hizi mpya dhidi ya walinda amani wake.

 

Uchunguzi huu unafanyika ikiwa ni mwezi mmoja tu umepita toka maofisa wa jamhuri ya Afrika ya Kati, wathibitishe kubaini matukio mapya zaidi ya 7 yanayowahusisha askari wa kulinda amani nchini humo wanaodaiwa kutekeleza vitendo vya udhalilishaji wa kingono.

Ad