Home » Afrika » Rais wa Malawi, Peter Mutharika amemjia juu muhubiri maarufu nchini Nigeria

Rais wa Malawi, Peter Mutharika amemjia juu muhubiri maarufu nchini Nigeria

14 March 2016 | Afrika

Rais wa Malawi, Peter Mutharika amemjia juu muhubiri maarufu nchini Nigeria, aliyedai hivi karibuni wakati wa utabiri wake, kuwa kiongozi huyo atafariki dunia kabla ya April Mosi mwaka huu.

Rais Mutahrika amesema kuwa, amepokea taarifa kuhusu unabii wa muhubiri huyo aliyemtaja kwa jina la TB Joshua, ambaye alifanya unabii kuwa yeye pamoja na rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe watakufa kabla ya April Mosi.

Mwaka 2012, muhubiri huyo, alitabiri kuhusu kutokea kwa kifo cha rais mmoja wa nchi iliyoko kusini mwa Afrika, ambapo kaka yake na Peter, Bingu wa Mutharika alifariki dunia.

Akiwahutubia maelfu ya wafuasi wake mjini Lilongwe, rais Mutharika ameseama kuwa safari hii, nabii huyo hatafanikiwa.

Ad