Home » Afrika » Rais wa Iran Hassan Rouhani taifa lake liko tayari kuurejesha ukurasa mpya

Rais wa Iran Hassan Rouhani taifa lake liko tayari kuurejesha ukurasa mpya

28 January 2016 | Afrika

Rais wa Iran Hassan Rouhani amesema taifa lake liko tayari kuurejesha ukurasa mpya wa ushirikiano wa kidiplomasia na Ufaransa, na hii baada ya kufikiwa kwa makubaliano ya kihistoria ya kudhibiti mpango wa nyuklia wa Iran ili nchi hiyo iondolewe vikwazo ilivyowekewa na mataifa ya magharibi.

Rouhani amewasili Paris hapo jana jumatano akitokea mjini Roma, wakati hafla rasmi ya kumkaribisha imefanyika leo asubuhi ikulu ya Elysée.

Imearifiwa kuwa rais huyo wa Iran atakutana na maafisa kadhaa wa serikalini na hali kadhalika viongozi wengine kabla ya kuwa na mazungumzo na rais Francois Hollande wa Ufaransa ambapo kwa pamoja watasimamia hafla ya kusainiwa kwa mikataba 20 baina ya nchi hizo mbili.

Ad