Home » Afrika » Polisi nchini Uganda wamelazimika kutumia mabomu

Polisi nchini Uganda wamelazimika kutumia mabomu

15 February 2016 | Afrika

Polisi nchini Uganda wamelazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wafuasi wa Mgombea urais wa chama cha upinzani cha FDC nchini Uganda Kizza Besigye ambaye alikamatwa na kuzuiliwa kwa muda na maafisa wa polisi mjini Kampala.

Kwa mujibu wa AFP Besigye,ambaye kwa mara tatu mfululizo ameangushwa katika uchaguzi na raisi museven alikamatwa na polisi baada ya kufanya kampeni zake mjini kampala huku msafara wake ukisindikizwa na mamia ya wafuasi, ndipo walipotumia mabomu ya machozi kuwatawanya wafuasi hao na kukamkamata mwanasiasa huyo.

Hata hivyo aliachiliwa huru bila kufunguliwa mashtaka baada ya kuzuiliwa kwa muda katika kituo cha polisi cha Kira Road.

Msema ji wa chama cha FDC Semujju Nganda amedai baadhi ya wafuasi wa chama chake walijeruhiwa katika rabsha rabsha za polisi.

Ad