Home » Afrika » NAIROBI; mwanamke mja mzito ameokolewa akiwa hai.

NAIROBI; mwanamke mja mzito ameokolewa akiwa hai.

05 May 2016 | Afrika

Baada ya siku sita kufunikwa na vifusi vya jengo la makaazi ya orofa saba liliporomoka katika mtaa wa Huruma jijini Nairobi nchini Kenya, mwanamke mja mzito ameokolewa akiwa hai.

Maafisa wa uokoaji wanasema yuko hospitalini anakoendelea kupata matibabu pamoja na kwamba hakuumia hata kidogo.

Mapema wiki hii, mtoto wa mwaka mmoja pia aliokolewa akiwa mzima.

Hata hivyo, idadi ya watu waliopoteza maisha imefikia 36.

Ad