Home » Afrika » Mohammed Alloush anasema hana matumaini ya kupatikana kwa mwafaka

Mohammed Alloush anasema hana matumaini ya kupatikana kwa mwafaka

03 February 2016 | Afrika

Mwakilishi wa upinzani katika mazungumzo ya amani ya Syria Mohammed Alloush anasema hana matumaini ya kupatikana kwa mwafaka baada ya mazungumzo hayo kuanza jana mjini Geneva nchini Uswizi.

Kiongozi huyo wa upinzani amesema kuwa haitawezekana wao kama wapinzani kuunda serikali ya umoja wa washirika wa karibu wa rais Bashar Al Assad.

Alloush, ameongeza kuwa haiwezi wao kuingia katika muunganano na watu ambao amewaalezea kuwa wanaendelea kuwauwa watoto wao.
Aidha, ameishtumu Urusi kwa kuendelea kumuunga mkono rais Assad na kuendeleza mashambulizi katika ngome zao.

Wakati hayo yakijiri jeshi la serikali limezingira mji wa Allepo ambao umekuwa ngome ya waasi huku, waasi hao wakilalamikia jeshi la Urusi kuendeleza mashambulizi hatua ambayo inahatarisha mazungumzo ya amani.

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa anayeongoza mazungumzo hayo  Staffan de Mistura ameekuwa akisema mazungumzo hayo yanalenga kumaliza mzozo wa Syria amabo sasa umedumu kwa miaka mitano na kusababisha maelfu ya watu kupoteza maisha na Mamilioni kuyakimbia makwao.

Ad