Home » Afrika » Kitengo cha intelijensia Drc kimemuachilia huru Martin Fayulu

Kitengo cha intelijensia Drc kimemuachilia huru Martin Fayulu

15 February 2016 | Afrika

Kitengo cha intelijensia ya jeshi nhcini Drc kimemuachilia huru kiongozi wa chama cha siasa cha upinzani Martin Fayulu, baada ya kumkamata mapema Jumapili kwenye makao makuu ya chama chake mjini Kinshasa.

Kiongozi wa chama cha ECIDE, akiwa pia mjumbe wa muungano wavyama vya upinzani na mgombea urais, Martin Fayulu aliwatolewa wito wafuasi wake kususia shughuli mbalimbali Februari 16 akidai uchaguzi ufanyike ndani ya muda uliopangwa kikatiba, kuheshimu Katiba na kanuni za kupishana madarakani kidemokrasia.

Mbunge Martin Mayulu alirudishwa nyumba kwake chini ya ulinzi mkali baada ya kuzuiliwa kwa saa kadhaa, licha ya kuwa na kinga ya ubunge. Martin Fayulu alikamatwa akiwa kwenye makao makuu ya chama chake alipokuwa akijiandaa kwa kampeni ya kuhamasisha wafuasi wake kuhusu maandamano ya siku ya Jumanne wiki hii.

Mbunge huyo wa upinzani ameiambia RFI kwamba alikamatwa katika mazingira ya vurugu na.

Baada ya kupelekwa katika ofisi za Idara ya upelelezi wa kijeshi, Martin Fayulu hatimaye alipewa fursa ya kukutana na mwanasheria wake. Msemaji wa serikali alitangaza kuachiliwa kwake kwenye majira ya saa mbili usiku,saa moja baada ya kuzuiliwa.

Ad